Aliye mbele ya wenzake hapo katika picha hii ndiye mkuu wa chuo cha ruaha catholic university FATHER.DR.CEPHAS MGIMWA,akifungua mashindano ya bonanza.Nyuma yake nibaadhi ya wafanya kazi kushoto ni Mpharmacia Goodluck Mdugi,anayefuata ni mwanassheria wa chuo,anayefuata ni Mpharmacia Gasper Baltazar.Anayefuata ni waziri wa michezo katika serikali ya wanafunzi RUCUSO,anayefuata ni Mwenyekiti wa TAPSA-RUCU mheshimiwa Samweli Musa,na mwisho ni naibu waziri wa michezo.
Kila mmoja aliye hudhuria alifurahi sana,siku hii ni moja ya siku ambayo haita sahaurika kwa wanafunzi wa shule ya dawa RUCU.Shukrani kwa viongozi wa TAPSA chini ya uongozi wa mheshimiwa Samweli Musa.Shukrani sana kwa katibu wa TAPSA aliye andaa mashindano hayo.
Dhumuni kubwa la kuweka tukio hilo,Kwanza ilikuwa ni kuongeza mahusiano na ushirikiano mzuri baina ya wanafunzi,pia ilikuwa nisiku maalumu yakuwa pamoja na dada na kaka zetu wanao maliza katika semister hii.Ilikuwa nisiku ya kuwaaga kabla hatujawafanyia sherehe yao tarehe 27/6/20015.Tunawashukuru sana DPS III kwa kujitokeza na kukubali kushiriki nasi siku hiyo.
MATOKEO
Vijana wa DPS II na DPS III hawata sahau kwa kichapo kikali walichopata toka DPS I
DPS I vs DPS II : 3-0
fainali
DPS I vs DPS III : 3-2
kikosi cha DPS I wababe wa DPS II na DPS III
Mashindano ya kuvuta kamba,kushoto ni DPS II na kulia ni DPS I
mwanafunzi wa DPS I akipiga danadana na ndio alikuwa mshindi wetu wa siku hiyo.
Miongoni mwawashindani wa danadana za kichwa DPS I
Miongoni mwa washindani wa mashindano ya mbio za magunia
Baadhi ya vijana wa DPS wakishuhudia michuano
Hiyo ni baadhi ya matukio yaliyo tukia siku hiyo.Baada ya mashindano hayo washindi walizawadiwa zawadi zao.Tunawashukuru sana waalimu wetu kwa kuwakaribu yetu na kwa kutujali pia.Kiukweli tunawapenda sana.Baadhi ya waalimu waliokuwepo siku hiyo ni pamoja na Mpharmacia mheshimiwa Gasper Baltazar na Mpharmacia mheshimiwa Goodluck Mdugi.Mungu awabariki sana.
Zawadi zikitolewa kwa washindi.Zoezi hilo liliongozwa na Mpharmacia mheshimiwa Gasper Baltazar kutoka kulia mtu wa tatu.
Tunawashukuru sana wanafunzi kwa kuonyesha ushirikiano mzuri na viongozi,Viongozi tunaahidi tutajitahidi kufanya kila mmoja kuona thamani ya chama chetu,tuzidi kushirikiana na kupendana pia.
DPS III KWAKHERINI TUNAWASHUKURU KWA KUWA KARIBU YETU.TUNAWAOMBENI TAREHE 27/6/2015 ASIKOSE MTU,NJOONI TUFURAHI PAMOJA KWASABABU SIKU HIYO NI MAALUMU KWA AJILI YENU.
TAFADHALI POPOTE MUENDAPO MSISAHAU KUWA
WELFARE OF HUMANITY AND RELIEF OF HUMAN SUFFERING IS OUR PRIMARY CONCERNS"
|
No comments:
Post a Comment